


Hadithi inaanzia mwaka 1980, ambapo Alex Mason na Frank Woods wanashiriki operesheni za kijeshi katika kipindi cha Vita Baridi. Wakiwa kwenye misheni zao, wanakutana na mtu hatari anayeitwa Raul Menendez, ambaye baadaye anakuwa adui mkubwa wa Marekani. Miaka inapita na simulizi linaendelea hadi mwaka 2025. Safari hii unacheza kama David Mason, mtoto wa Alex Mason, ambaye anaongoza operesheni za kukabiliana na Menendez. Menendez amekuwa kiongozi wa kundi lenye nguvu la kigaidi linaloitwa Cordis Die. Ana mpango wa kutumia teknolojia ya kijeshi na mashambulizi ya mtandaoni kusababisha machafuko duniani na kulipiza kisasi dhidi ya Marekani. Kadiri operesheni zinavyoendelea, unakutana na maamuzi magumu ambayo yanaweza kubadilisha mwelekeo wa hadithi na hatima ya wahusika.