


Wewe unacheza kama Bearer of the Curse, shujaa anayesafiri mpaka ufalme ulioanguka wa Drangleic, akitafuta njia ya kuondokana na laana hiyo. Huko unakutana na historia ya King Vendrick, mfalme mwenye nguvu aliyewahi kuitawala Drangleic, lakini ufalme wake uliangamia baada ya vita na ushawishi wa malkia Nashandra, ambaye alikuwa na malengo yake ya siri. Ili kufikia ukweli, unatakiwa kukabiliana na maadui wa kutisha, majitu, mashujaa waliolaaniwa na kukusanya roho nne zenye nguvu. Kinachofanya Dark Souls 2 kuwa game la kipekee ni kwamba kifo si mwisho. Kila unapokufa, unarudi tena, lakini laana inaendelea kukuathiri. Na mwisho wa safari, unakabiliwa na swali kubwa: Je, utachukua kiti cha enzi na kuendeleza mzunguko wa dunia, au utatafuta njia nyingine ya kuuvunja?