Inapakia games za PC…



Silent Hill 2 ni mchezo wa kutisha wa kisaikolojia (Psychological Horror) unaomfuata James Sunderland, mwanaume anayepokea barua ya ajabu kutoka kwa mke wake Mary, ambaye alifariki miaka mitatu iliyopita. Barua hiyo inamwambia James arudi katika mji wa Silent Hill, mahali walipowahi kutembelea pamoja. Akiwa na matumaini ya kumpata mke wake, James anasafiri hadi mji huo, lakini anakuta umefunikwa na ukungu mzito na umejaa viumbe vya kutisha. Katika safari yake, James anakutana na watu wenye historia za kutisha pamoja na monster hatari anayejulikana kama Pyramid Head. Kadiri anavyoendelea kuchunguza mji, anaanza kugundua ukweli wa kutisha kuhusu kifo cha mke wake, hatia aliyoificha na kumbukumbu zinazomtesa.