


Where Winds Meet ni game ya Action RPG inayokupeleka katika China ya kale, kipindi cha karne ya 10, ambapo vita, usaliti, siasa na mapambano ya madaraka vinatawala. Unacheza kama mpiganaji kijana mwenye ujuzi mkubwa wa martial arts, anayeishi katika dunia ambayo kila mtu anapigania nguvu, mamlaka na heshima. Safari yako inaanza ukiwa unatafuta kujua ukweli kuhusu maisha yako na siri zilizofichwa katika historia ya nchi yako. Lakini kadri unavyoendelea na safari, unajikuta katikati ya migogoro mikubwa kati ya falme, makundi ya wapiganaji na watu wenye nguvu wanaotaka kuitawala China. Utapambana na maadui wenye uwezo wa ajabu, utajifunza mitindo mbalimbali ya mapigano, na kufanya maamuzi yatakayoathiri safari yako. Kinachofanya game hii iwe kali ni kwamba wewe si mpiganaji tu, bali wewe ndiye unayeamua utakuwa shujaa, muuaji au mtu atakayebadilisha historia.