


Siku moja, Wolf anashindwa kwenye mapambano dhidi ya Genichiro Ashina, anayemkata mkono na kumteka Kuro ili kutumia nguvu zake kuokoa ukoo wa Ashina. Wolf anaokolewa na mchongaji wa sanamu anayempa mkono wa bandia wa Shinobi, wenye silaha mbalimbali. Hapo ndipo safari yake inaanza ya kupambana na Samurai, Shinobi na viumbe wa kutisha ili kumwokoa Kuro. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba Wolf anaweza kufa na kufufuka tena, kutokana na nguvu alizopewa na Kuro. Kadiri anavyoendelea na safari, anagundua kuwa nguvu ya kutokufa imeleta mateso na laana kwa watu wengi. Kuro anaamua kuvunja urithi huo wa kutokufa, na Wolf lazima amsaidie. 🔥 Kinachofanya Sekiro kuwa ya kipekee ni mfumo wake wa mapigano unaohitaji timing, parrying na ustadi mkubwa. Huwezi kushinda kwa kubonyeza vitufe hovyo!